Tunatoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa mtu mmoja mmoja na vikundi mbalimbali vyakijamii na vyakifedha kama vile vikoba ili kuwajengea fikra, uthubutu wa fikra, uwezo na umahiri wakufanya shughuli za uzalishaji ili kuongeza vipato vyao. Halikadhalika, tunafundisha juzi mbalimbali za kutengeneza bidhaa tofautitofauti zikiwemo; bidhaa za ngozi, waini, sabuni, bidhaa za ukili, nakadhalika. Pia tunafundisha kwa nadharia na vitendo ya masoko na mauzo ya bidhaa
Tunatoa Elimu ya Fedha kwa mtu mmoja mmoja na vikundi vya kijamii na kifedha ili kuwajengea uwezo wa kupata pesa na kuzitumia kimkakati na kuleta maendeleo katika hali zao za kiuchumi, namna ya kuhifadhi fedha, kukuza mtaji, kukopa, kujikinga na majanga, kodi, kutunza kumbukumbu za biashara na kupanga maisha ya uzeeni ili usiwe tegemezi katika maisha yako ya uzeeni na kadhalika
Tunatoa huduma ya mafunzo kwa vitendo kwakuwaruhusu wajasiriamali/mtu au kikundi cha watu wanaotaka kujifunza kwa vitendo ujuzi fulani kushiriki katika miradi yetu mbalimbali kwa muda maalumu. Washiriki watapatia mafunzo hayo hatua kwa hatua toka mwanzoni mwa mradi mpaka mwisho. Kisha wanaweza kuanzisha miradi yao yenye kufanana na ile waliojifunza kwa vitendo toka kwetu na GPOINT itawaongoza mpaka pale watakapoona wanaweza kuendelea wenyewe bila muongozo wetu
Unahitaji kujiunga katika Familiya ya Wajasiriamali wa GPOINT?