KUHUSU SISI

Gpoint Development Consultancy (GPOINT) ni kampuni ya kizalendo inayolenga kuinua maisha ya Wanawake na Vijana wa hali ya chini na yakati kiuchumi kupitia Ujasiriamali.

GPOINT inaamini katika Ujasiriamali kama njia ya kweli na sahihi yakupambana na umasikini. Hii ni kweli kama Elimu sahihi ya Ujasiriamali itatolewa ikiambatana na Elimu ya Fedha. Elimu hizi zitolewe kwa namna ambayo itamfikia mtu wa hali ya chini kabisa.

Mbali na kutoa Elimu ya Ujasiriamali na Fedha, GPOINT pia inatoa mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali ikilenga kumpatia mjasiriamali uwezo wa kutengeneza bidhaa hizo, kwakuzingatia ubora,masoko na mauzo.

Halikadhalika, inatoa fursa kwa wajasiriamali kujifunza kwa vitendo kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na GPOINT na baadaye kusimamia miradi itakayoanzishwa na wahitimu wa mafunzo hayo shirikishi ya vitendo mpaka pale watakapoweza kujisimamia wenyewe.